MY SCRIPTS



JITAA



IMEANDIKWA NA



ERICK MACHUA


MUSICAL DRAMA
























P.O.BOX 477
ARUSHA
TANZANIA












fade in

nje.jioni.barabarani
Watu wanaonekana wakiwa wenye haraka.Ni muda ambao watu wametoka kwenye shughuli zao za siku (Rush hours)
(Sauti ya jitaa inasikika likipigwa taratibu)
cut to
nje.jioni.nyumbani kwa mr adam
Ni jumba kubwa la kifahari.Taa za nje zinaongeza uzuri wa bungaloo hili.Getini gari linaingia taratibu.Taratibu linapaki kando ya magari mengine ya kifahari.
(Sauti ya jitaa bado inasikika)
Mr Adam (59) anashuka kwenye gari akiwa amevalia suti nyeusi.Ni mzee Mnene na Mrefu kiasi.Anaangalia huku na huko kisha anaelekea mlango wa sebuleni.
cut to
ndani.jioni.nyumbani kwa mr adam.sebuleni
TV inawaka.Hakuna mtu sebuleni.Kwenye TV ni ya mziki inachezwa.
(Sauti ya jitaa bado inasikika.Inaingiliana na Sauti ya mziki kwenye TV)
Mr Adam anatingisha kichwa kwa masikitiko.Anaelekea kwenye kordo fupi.Sauti ya jitaa inasikika toka chumba kimojawapo.Anafungua mlango wa chumba hicho.Ima (Emmanuel) (19) anaonekana amekaa juu ya kitanda akipiga jitaa bila kufahamu baba yake anamuangalia kwa mlangoni.Mr Adam anafunga mlango na kuelekea chumbani kwake.Ima anaacha kupiga jitaa baada ya kusikia kama mlango wa chumbani kwake umeguswa.Anaangalia mlangoni.
cut to
ndani.jioni.chumbani kwa mr adam
Mrs Adam (56)anaonekana akipanga nguo kwenye kabati.Anageuka baada ya mlango kufunguliwa na Mr Adam kuingia.Mr Adam anakaa kwenye kochi na kuanza kufungua tai yake.

MR.ADAM
Umeshindaje?
mrs.adam
Salama, za kazi?
mr adam
Ah mambo yameenda vizuri ila wale jamaa wa Malawi ndo wanaonekana hawako tayari.
mrs adam
Wana wasiwasi gani?
mr adam

Ah! hata nikikuelezea huwezi ukaelewa.ni complicated kidogo…Anna hajafika bado?
MRS ADAM
Bado…ila atakuwa njiani
mr adam
Mbona imechukua muda hivyo?
mrs adam
Nilimuomba apitie kwa shangazi yangu aje na yule housegirl
mr adam
(kwa hasira kidogo)
Ah…hivi umeshakaa na Ima ukaongea nae?...mimi nikiongea nae

(continued)
CONTINUED:
nitakasirika tu..atanipandisha presha.
mrs adam
Baba Chriss..ni jana tu umeniambia niongee nae…leo nilikuwa nashunguli nyingine sijaweza kukaa hata chini.

No comments:

Post a Comment