[Jay] All I need in this life of sin, is me and my girlfriend.
[Bey] Down to ride 'til the very end, it's me and my boyfriend.
[Jay] All I need in this life of sin, is me and my girlfriend.
[Bey] Down to ride 'til the very end, it's me and my boyfriend.
[Bey] Down to ride 'til the very end, it's me and my boyfriend.
[Jay] All I need in this life of sin, is me and my girlfriend.
[Bey] Down to ride 'til the very end, it's me and my boyfriend.
Hiki ni kiitikio cha wimbo maarufu wa msanii Jay z akiwa na mkewe Beyonce.Wimbo wenyewe unaitwa Bonnie and Clyde(Ama wengine wakiuuita Me and my Girlfriend).Ukiangalia mashairi ya kiitikio hiki kwa harakaharaka hayatakuvutia kutokana na ujumbe uliomo ndani yake.(Hasa kama wewe ni muumini mzuri wa Dini).Kwa tafsiri rahisi ya kiswahili yaweza kuleta maana hii.
[Jay]Nachohitaji katika maisha haya ya dhambi,ni mimi na msichana wangu
[Bey]Kwanzia mwanzo mpaka mwisho,ni mimi na mvulana wangu
[Jay]Nachohitaji katika maisha haya ya dhambi,ni mimi na msichana wangu
[Bey]Kwanzia mwanzo mpaka mwisho,ni mimi na mvulana wangu
Wakiimba kwa kupokezana Jay z anasema anachohitaji katika maisha haya ya dhambi ni msichana wake(mpenzi) na Beyonce anaitikia kwa kusema kwanzia mwanzo mpaka mwisho ni yeye na mvulana wake(mpenzi).
Historia ya wimbo huu ni ndefu ingawa muda haujafifisha umaarufu wake.Wengi hawafahamu undani wa wimbo huu.Kwa wale marahibu wa filamu(yaani wapenzi wakupindukia wa filamu)wanaweza wakawa wanafahamu Historia ya Bonnie and Clyde.Hata wale wafuatiliaji wazuri wa Historia wanaweza wakawa wanafahamu pia.
Bonnie Elizabeth Parker na Clyde Chestnut Barrow walikuwa majambazi na wahalifu maarufu kutoka Dallas huko Marekani wakisafiri kutoka katikati ya Marekani kipindi cha mtikisiko mkubwa wa uchumi(Great Depression).Bonnie na Clyde walikuwa wapenzi.Walisafiri pamoja na kundi lililokuwa likifanya uhalifu kwa kuiba Supermarkets na vituo vya mafuta.Inaaminika kundi hili liliua zaidi ya watu tisa.
Bonnie Parker
Huyu ni mwanadada.Alizaliwa mwaka 1910 akiwa mtoto wa pili kati ya watatu ya Charles Parker.Bonnie alikuwa kati ya watoto waliofanya vizuri shuleni akifaulu vyema katika masomo ya
kuandika,herufi na kuongea mbele ya halaiki.Upenzi wake wa kuandika akiwa mtu mzima ulimfanya kuanza kuandika mashairi na miongoni ya mashairi yake ni "The Story of Suicide Sal"na "The Trail's End" (ambayo pia hujulikana kama "The Story of Bonnie and Clyde"
Katika mwake wake wa pili wa Sekondari alikutana na Roy Thornton na wakaacha shule ambapo baadae walioana.Ndoa hii haikudumu kwa muda mrefu kutokana na matatizo kadha wa kadha yaliyopelekea kutengana ingawa hawakutalakiana.
CLYDE BARROW
Clyde aliyezaliwa mwaka 1909 alikuwa muhalifu wa kupindukia katika umri mdogo.Dada yake alikaririwa akisema "kitu fulani lazima kilimtokea akiwa gerezani maana baada ya kutoka hakuwa wa kawaida"Rafiki yake naye alikaririwa akisema alimuona akibadilika kutoka mvulana wa shule na kuwa Nyoka wa kutisha.Alianza kuiba Maduka makubwa,vituo vya mafuta na Mabenki na alitumia silaha aina ya M1918 Browning Automatic Rifle ambayo ni bunduki.Yote haya aliyafanya akiwa na kundi lake la Barrow.Inasemekana Clyde alifanya uhalifu huo sio kwa ajili ya kupata pesa ama kutajirika bali kulipiza kisasi kutokana na mateso aliyoyapata akiwa gerezani.
KUKUTANA KWA BONNIE NA CLYDE
Bonnie na Clyde walikutana katika nyumba ya Clarence(ambaye ni rafiki wa Clyde) na mara moja wakapendana na walibaki kuwa wapenzi walioshibana mpaka kifo walichodhani hakitoweza kutokea kilipowatenganisha.
UHALIFU
Wakiwa pamoja walifanya uhalifu mkubwa wa kuiba mabenki,magari,maduka,migahawa pamoja na vituo vya mafuta pamoja na kuua watu.Katika kufanya uhalifu huo mwanakundi mwenzao aliyeitwa Bucher aliuliwa na kipindi fulani Boniie alifungwa jela lakini akaweza kutoka baada ya muda mfupi.Akiwa gerezani aliandika mashairi kadhaa.
PICHA MAARUFU YA BONNIE AKIWA ANAVUTA
HUKU AMESHIKILIA BASTOLA MKONONI.
Kumbuka hiki kilikuwa kipindi cha mtikisiko mkubwa wa uchumi(1929-1939) na kundi hili lilifanya uhalifu bila huruma huku wakitumia silaha ambazo zilikuwa na uwezo mkubwa kuliko mapolisi.Kuna kipindi yalitokea mapambano ya kurushiana risasi kati ya kundi la Barrow na Polisi ambapo polisi mmoja laiuliwa huku mwingine akijeruhuliwa vibaya.Hii inaonesha ni jinsi gani kundi hili lilikuwa tishio.
Mwaka 1933 mwezi wa nne tarehe 13 polisi walizingira nyumba ya gereji walimokuwa wamejificha Clyde na wenzake tayari kuwakamata.Clyde na wenzake walishtukia mbinu hiyo na majibizano ya risasi yalitokea.Cha ajabu polisi walizidiwa kete baada ya kundi la Barrow kufanikiwa kutoroka na kuwaacha polisi kwenye mataa huku polisi mmoja akiwa ameuliwa Katika majibizano hayo ya risasi
huku Clyde na wenzake wawili wakijeruhuliwa kidogo.Polisi walifanikiwa kukusanya baadhi ya vitu walivyoviacha akina Clyde mara baada ya kutoroka ikiwemo kamera na karatasi yenye shairi aliloandika Bonnie.Picha zilizokuwa kwenye kamera zilisafishwa na mojawapo ndo hiyo ya Bonnie akiwa anavuta sigar huku akiwa ameshikilia bastola mkononi.Picha hizo ziliwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti zikitangaza kuwa ni wahalifu hatari wa Amerika.Shahiri lililokamatwa la The Story of Suicidal Sal lilijizolea umaarufu mkubwa.Kwa miezi mitatu baadae kundi hili lilifanya uhalifu mkubwa sehemu za Texas,Minnesota na Indiana.Kundi hili likawa gumzo kila mahali na hatari kwa jamii.Mwaka huohuo mwezi wa sita Clyde na Bonnie walipata ajali baada ya gari lao kupinduka na Bonnie akaumia vibaya mguu wake wakulia hali iliyompatia kilema.Hakuweza tena kutembea vizuri na mara yingine Clyde alimbeba.Mwezi wa Saba tarehe 18 Clyde na kundi lake lilijificha sehemu moja iliyoitwa Red Crown tourist Court huko Missouri.Baada ya uwepo wao kugundulika hapa polisi walizingira nyumba waliyopanga wakiwa na silaha hatari.Hapa tena mapambano yalitokea.Hapa walifanikiwa kutoroka tena ila safari hii wakimuacha mwenzao mmoja ambaye alikamatwa na polisi.
![]() | ||
Blanche mmoja wa genge la Barrow akiwa amekamatwa baada | ya wenzake kufanikiwa kutoroka. |
Mwaka 1934 mwezi wa kwanza tarehe 16 Clyde alipanga mpango wa kuwatorosha wafungwa maarufu.Mpango huo ulifanikiwa na hii ikawa aibu kwa Jimbo la Texas.Hii ilifanya Bonnie na Clyde kuwa wafungwa wanaotafutwa kwa udi na uvumba.Idara ya Texas ilimtafuta polisi mstaafu Frank Hamer ili kuwasaka Clyde na kundi lake.Ingawa Hamer alikuwa mstaafu alikubaliana na kazi hiyo.Hamer alikuwa askari anayeigopeka kwa mambo mwengi na alikuwa mchapa kazi na mwenye nguvu,ujuzi na akili.Alipata umaarufu usiohojika kutokana na kufanikiwa kukamata baadhi ya wahalifu tishio.Hivyo ilionekana kazi ya kuwatia nguvuni Clyde na wenzake ingemfaa.Kazi hii haikuwa rahisi kama Hamer alivyofikiri.Kundi liliendelea kuua na kuteka watu.Raia nao walijawa na jazba na kuona polisi hawafanyi kazi.Hali haikuwa nzuri huko Texas.
Hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho.Tarehe 23 Mwezi wa Tano mwaka 1934 Hamer aliwapanga askari wake vizuri katika eneo la maficho kichakani.Akijua kuwa Bonnie na Clyde watapita njia hiyo.Baada ya Subira ndefu walisikia gari la Clyde likiunguruma kwa mbali.Gari aina ya Ford V8 lililoibiwa siku si nyingi.Askari hao wanasema Clyde alisimamisha gari ili kuongea na Baba wa Methvins(Methvins alikuwa Rafiki wa Clyde) ambaye alikuwa ameegesha lori lake barabarani.Baba wa Methvins alikuwa amewekwa pale kwa makusudi ili Clyde asimamishe gari.Hilo lilifanikiwa na askari waliokuwa mafichoni walimimina risasi kama mvua kwenye gari la Clyde.Risasi hizo zilizotoboa gari la Clyde kama chekecheke zilitosha kukatisha maisha ya wapenzi hao wahalifu.Huo ukawa mwisho wa maisha ya Bonnie na Clyde.
Wachambuzi wanasema Bonnie na Clyde walipigwa Risasi zaid ya hamsini.Kidoleni Bonnie alikuwa bado amevaa pete ya arusi aliyofunga na Roy(Mwanamume aliyefunga naye ndoa kabla hajakutana na Bonnie.
MSIBA NA MAZISHI
Bonnie na Clyde walitaka kuzikwa pamoja.Ila familia ya Bonnie ilikataa jambo hilo.Bonnie alizikwa huko Dallas katika makaburi ya Crown Hill huku Clyde akizikwa makaburi ya Western Height hukohuko Dallas.Shairi hili ni ishara kuwa Bonnie na Clyde walitaka kuzikwa pamoja.Bonnie alitabiri pia watakufa pamoja.
The Story of Bonnie and Clyde
You've read the story of Jesse James
Of how he lived and died;
If you're still in need
Of something to read,
Here's the story of Bonnie and Clyde.
Now Bonnie and Clyde are the Barrow gang,
I'm sure you all have read
How they rob and steal
And those who squeal
Are usually found dying or dead.
There's lots of untruths to these write-ups;
They're not so ruthless as that;
Their nature is raw;
They hate all the law
The stool pigeons, spotters, and rats.
They call them cold-blooded killers;
They say they are heartless and mean;
But I say this with pride,
That I once knew Clyde
When he was honest and upright and clean.
But the laws fooled around,
Kept taking him down
And locking him up in a cell,
Till he said to me,
"I'll never be free,
So I'll meet a few of them in hell."
The road was so dimly lighted;
There were no highway signs to guide;
But they made up their minds
If all roads were blind,
They wouldn't give up till they died.
The road gets dimmer and dimmer;
Sometimes you can hardly see;
But it's fight, man to man,
And do all you can,
For they know they can never be free.
From heart-break some people have suffered;
From weariness some people have died;
But take it all in all,
Our troubles are small
Till we get like Bonnie and Clyde.
If a policeman is killed in Dallas,
And they have no clue or guide;
If they can't find a fiend,
They just wipe their slate clean
And hand it on Bonnie and Clyde.
There's two crimes committed in America
Not accredited to the Barrow mob;
They had no hand
In the kidnap demand,
Nor the Kansas City depot job.
A newsboy once said to his buddy;
"I wish old Clyde would get jumped;
In these awful hard times
We'd make a few dimes
If five or six cops would get bumped."
The police haven't got the report yet,
But Clyde called me up today;
He said, "Don't start any fights
We aren't working nights
We're joining the NRA."
From Irving to West Dallas viaduct
Is known as the Great Divide,
Where the women are kin,
And the men are men,
And they won't "stool" on Bonnie and Clyde.
If they try to act like citizens
And rent them a nice little flat,
About the third night
They're invited to fight
By a sub-gun's rat-tat-tat.
They don't think they're too tough or desperate,
They know that the law always wins;
They've been shot at before,
But they do not ignore
That death is the wages of sin.
Some day they'll go down together;
And they'll bury them side by side;
To few it'll be grief
To the law a relief
But it's death for Bonnie and Clyde.
![]() |
ASKARI WALIOTEKELEZA MAUAJI YA BONNIE NA CLYDE |
![]() |
GARI WALIMOKUWAMO BONNIE NA CLYDE BAADA YA KUMIMINIWA RISASI |
MSIBA NA MAZISHI
Bonnie na Clyde walitaka kuzikwa pamoja.Ila familia ya Bonnie ilikataa jambo hilo.Bonnie alizikwa huko Dallas katika makaburi ya Crown Hill huku Clyde akizikwa makaburi ya Western Height hukohuko Dallas.Shairi hili ni ishara kuwa Bonnie na Clyde walitaka kuzikwa pamoja.Bonnie alitabiri pia watakufa pamoja.
The Story of Bonnie and Clyde
You've read the story of Jesse James
Of how he lived and died;
If you're still in need
Of something to read,
Here's the story of Bonnie and Clyde.
Now Bonnie and Clyde are the Barrow gang,
I'm sure you all have read
How they rob and steal
And those who squeal
Are usually found dying or dead.
There's lots of untruths to these write-ups;
They're not so ruthless as that;
Their nature is raw;
They hate all the law
The stool pigeons, spotters, and rats.
They call them cold-blooded killers;
They say they are heartless and mean;
But I say this with pride,
That I once knew Clyde
When he was honest and upright and clean.
But the laws fooled around,
Kept taking him down
And locking him up in a cell,
Till he said to me,
"I'll never be free,
So I'll meet a few of them in hell."
The road was so dimly lighted;
There were no highway signs to guide;
But they made up their minds
If all roads were blind,
They wouldn't give up till they died.
The road gets dimmer and dimmer;
Sometimes you can hardly see;
But it's fight, man to man,
And do all you can,
For they know they can never be free.
From heart-break some people have suffered;
From weariness some people have died;
But take it all in all,
Our troubles are small
Till we get like Bonnie and Clyde.
If a policeman is killed in Dallas,
And they have no clue or guide;
If they can't find a fiend,
They just wipe their slate clean
And hand it on Bonnie and Clyde.
There's two crimes committed in America
Not accredited to the Barrow mob;
They had no hand
In the kidnap demand,
Nor the Kansas City depot job.
A newsboy once said to his buddy;
"I wish old Clyde would get jumped;
In these awful hard times
We'd make a few dimes
If five or six cops would get bumped."
The police haven't got the report yet,
But Clyde called me up today;
He said, "Don't start any fights
We aren't working nights
We're joining the NRA."
From Irving to West Dallas viaduct
Is known as the Great Divide,
Where the women are kin,
And the men are men,
And they won't "stool" on Bonnie and Clyde.
If they try to act like citizens
And rent them a nice little flat,
About the third night
They're invited to fight
By a sub-gun's rat-tat-tat.
They don't think they're too tough or desperate,
They know that the law always wins;
They've been shot at before,
But they do not ignore
That death is the wages of sin.
Some day they'll go down together;
And they'll bury them side by side;
To few it'll be grief
To the law a relief
But it's death for Bonnie and Clyde.
No comments:
Post a Comment