SAFARI YA MBUGANI.
Katika
kusheherekea mahafali ya kumaliza chuo kikuu,marafiki sita waliamua kwenda
kuweka kambi katika mbuga moja kama sehemu ya sherehe yao.Baada ya safari ya
masaa kadhaa kutoka mjini walifika katika mbuga hiyo.Walitafuta sehemu nzuri na
kuweka kambi yao.Walipoweka kambi palikuwa na bwawa dogo.Kwa mujibu wa taarifa
walizopewa mapokezi nk kwamba wangeweza kuogelea katika bwawa hilo kwani
halikuwa na hatari yoyote.Walitumia muda mwingi kuogelea na kucheza.Naam maji
yalikuwa matamu na mazuri.
Jua
lilipokuwa likiaga tayari walikuwa wamechoka hivyo walijipumzisha kwenye majani
wakijikumbushia mambo mengi ya chuo.Hadithi zao nyingi zilikuwa za kufurahisha
na kuchekesha.Mmmoja kati yao alipanda juu ya mwamba mkubwa uliokuwa karibu na
bwawa na kujirusha kwenye maji wakati wengine wakiangalia.Vicheko vyao vilianza
kufifia baada ya muda kupita bila rafiki yao kutoka ndani ya maji.Ghafla
wakajirusha kwenye majani ili kumtafuta rafiki yao.Walitafuta kwa muda mrefu
bila mafanikio.Hiyo ndo ilikuwa mwisho wa kumuona rafiki yo kipenzi.
Mwaka
ulipita na mioyo ikiwa imevunjika
walirudi mbugani kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya rafiki yao.Lakini
walipokaribia bwawa walishtushwa
kumuona mtu kama rafiki yao.Alikuwa amesimama kando ya bwawa.Walisogea
karibu.Fika alikuwa yeye.Walimuita lakini hakuitika.Walisogea karibu
zaidi.Walipomkaribia kwa namna ya
ajabu na ya kustaajabisha hawakumuona mtu zaidi ya mawimbi yakipepesa ndani ya maji.
No comments:
Post a Comment