Ilikuwa usiku kwenye majira ya saa tatu.Miaka kama mitatu iliyopita.Baba yangu(My Hero) Mzee christopher Machua aliingia ndani nakukuta tumekaa sebuleni mini na wadogo zangu."Erick umeshawahi kusikia kitu chochote kuhusu Bermuda Triangle?"Lilikuwa swali la kwanza mara baada ya kumsalimia na kukaa.Bermuda Triangle?.Nilijiuliza.Ilikuwa ndo mara ya kwanza kusikia hicho kitu.
"Hapana Baba"nilijibu kwa upole.
"Mnatakiwa mfahamu,hivi ni vitu muhimu sana kuvijua"Alisema kwa msisitizo.
"Ni nini hiyo Bermuda Triangle?"Nilimuuliza
Bila kuniangalia machoni "Tafuta,ni rahisi kupata"
Baada ya hapo tuliongea mambo mengine mengi ila akilini mwangu jina Bermuda Triangle lilikuwa likizunguka.What is this Thing called Bermuda Triangle.I could understand the word Triangle(pembe tatu).But Bermuda!..a lot of question marks.Siku hiyohiyo nilichukua simu yangu ya kiganjani(thanks for the internet thing wazungu wametuletea)na kuanza kuperuzi mtandao kuitafuta hii pembetatu iitwayo Bermuda.
Bermuda Triangle ambayo mimi nitaiita Pembe tatu ya Bermuda ambayo pia huitwa Pembetatu ya shetani ni eneo katika mashariki ya Bahari ya Atlantic kwa upande wa kaskazini ambapo inasemekana ndege na meli kadhaa zilishapotea katika mazingira ya kutatanisha.Ila kwa mujibu wa US Navy pembe tatu hii haipo na jina hili la Bermuda Triangle halitambuliwi na Bodi ya majina ya kijiografia ya Marekani.Watu wengi wamekuwa wakihusisha kupotea kwa meli ama ndege hizo na mambo ya kishetani ama mambo yasiyo ya kawaida.Mwaka 2013 mfuko maalum wa kimataifa kwa ajili ya mambo ya asili ulitaja sehemu kumi za maji zilizo hatari kwa meli lakini Pembe tatu ya Bermuda haikutajwa.Pembetatu ya Bermuda ina hadithi na simulizi nyingi.Wako wanaoziamini na wako wasioziamini.Kupotea kwa ndege ya Malaysia 370 tarehe 8 mwezi wa tatu 2014 kunanifanya niwe kwenye kundi la waaminio.Kwa kufuatilia kwa undani zaidi kuhusu Pembetatu ya Shetani Bonyeza hapa Bermuda Triangle
No comments:
Post a Comment