Wednesday, February 18, 2015

ELICE KATIKA NCHI YA AJABU

-->
Na Erick Machua

Alice’s adventures in wonderland (Alice In Wonderland)ni Riwaya iliyoandikwa na mwanariwaya maarufu wa kiingereza  Charles Lutwidge Dogson mwaka 1865.Ni hadithi inayomuelezea Binti aitwaye Alice aliyedumbukia kwenye shimo la sungura na kujukuta akitokea katika dunia nyingine ya ajabu na yenye viumbe visivyo vya kawaida.Ingawa Riwaya hii imejijenga zaidi katika mambo ya kusadikika imejipatia umaarufu mkubwa sana tangu ilipotolewa.Filamu mbalimbali zimepata kutolewa kutokana na Riwaya hii maarufu zikiwa zile za Alice in Wonderland (1903
Alice's Adventures in Wonderland (1910 na nyingine nyingi.Umaarufu wa kazi hii umepelekea kupatikana kwa msemo wa Alice in Wonderland.Msemo huu hutumika sehemu mbalimbali kuashiria kitu cha ajabu ama kisichoeleweka. Kwa mfano unaweza sema kwa kimombo “This-alice -in wonderland economic system”yaani kumaanisha uchumi usioeleweka.Au unaweza kusema kwa kwa Kiswahili rahisi “uchumi wa nchi yetu ni kama Alice kwenye nchi ya ajabu”

No comments:

Post a Comment